UTATUZI WA MIGOGORO KWA NJIA YA USULUHISHI NA UPATANISHI.βšͺ️

Ni wazi kwamba msisitizo umekuwa ukitolewa kwa wananchi kutoka mamlaka mbalimbali za vyombo vya dola kuhusu kutojichukulia Sheria Mkononi. Wananchi wamekuwa wakiaswa kufika mbele ya vyombo vya sheria kwa uamuzi ama utatuzi wa migogoro yao. Hata hivyo Leo njia ya utatuzi wa migogoro kwa UPATANISHI, USULUHISHI na UAMUZI nje ya mahakama umekuwa ukihamasishwa sana, katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye ngazi ya serikali za Vijiji na mabaraza ya kata. Njia hizi zina faida nyingi mno kwa wenye mgogoro na hata mahakama yenyewe kama ifuatavyo:

1. Njia hizi huokoa gharama ambazo zingetumika kama ada ya kusajili kesi mahakamani na nyinginezo kama usafiri wa mara kwa mara kuhudhuria kesi.

2. Kutunza hali ya maelewano baina ya wenye mgogoro na kuondoa uhasama, hii hutokana na ukweli kwamba njia hizi hazitafuti mshindi ila zina sawazisha kila upande hivyo hakutakuwa na kinyongo au kisasi baina yao,kwani hufanyika kirafiki zaidi.

3. Njia hizi hupunguza msongamano wa kesi mahakamani, kesi nyingi ambazo zingepelekwa mahakamani zitatatuliwa kwa njia hizi na kupunguza mlundikano wa kesi.

4. Njia hizi huokoa muda sana, muda wa usuluhishi ni mfupi zaidi kuliko muda wa kuendesha kesi mahakamani, kuendesha kesi ni mchakato mrefu sana unaoambatana na kutoa ushahidi na vielelezo vingi.

5. Njia hizi ni rahisi katika utendekaji wake haziusishi michatakato na matakwa mengi ya kisheria yanayolazimu kuweka wakili katika shauri fulani kwa sababu hufanyika kirafiki zaidi.

Kutokana na faida tajwa hapo juu ndio maana mkazo mkubwa umekuwa kusisitiza watu kutumia njia hizi zaidi. Ndio ilikuwa kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini Tanzania mwaka huu wa 2023.

Andiko na Richard Kalokola.

@richardkalokola


Discover more from π‹π„π†π€π‹π‰π€πŒπˆπˆβš–οΈ

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Published by LEGALJAMIIβš–οΈ

Richard Kalokola is a Tanzanian legal professional with a Bachelor of Laws (LL.B) from St. Augustine University of Tanzania and professional training from the Law School of Tanzania. He has a strong passion for legal education, research, and public legal awareness. As the founder of LegalJamii, Richard is dedicated to bridging the gap between complex legal principles and everyday understanding by delivering accurate, practical, and accessible legal information. His vision is to promote a legally informed society where individuals, businesses, and communities can confidently understand their rights, responsibilities, and available legal solutions. Through LegalJamii, he continues to advance legal literacy by transforming legal concepts into clear and simplified language for the benefit of the wider public.

Leave a Reply

Discover more from π‹π„π†π€π‹π‰π€πŒπˆπˆβš–οΈ

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Discover more from π‹π„π†π€π‹π‰π€πŒπˆπˆβš–οΈ

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading