POWER OF ATTORNEY TANZANIA: MAANA, MATUMIZI NA USAJILI

Na Richard Kalokola

Utangulizi

Katika maisha ya kila siku, kuna mazingira ambayo mtu anakuwa na shughuli muhimu za kisheria au kibiashara lakini hawezi kuzitekeleza mwenyewe. Anaweza kuwa yuko nje ya nchi, anaumwa, yuko mbali na eneo ambako shughuli inapaswa kufanyika, au ana majukumu mengine yanayomzuia kushughulikia jambo hilo binafsi.

Katika mazingira hayo, sheria inaruhusu mtu kumteua mtu mwingine kumwakilisha na kutekeleza shughuli fulani kwa niaba yake. Hapo ndipo dhana ya Power of Attorney (POA) inapopata umuhimu.

Kwa lugha rahisi, Power of Attorney ni hati ambayo mtu mmoja humpa mtu mwingine mamlaka ya kumwakilisha na kufanya vitendo au shughuli zilizotajwa katika hati hiyo kwa niaba yake.

Katika matumizi ya kisheria, mtu anayetoa mamlaka huitwa Donor, Grantor au Principal, wakati anayepokea mamlaka huitwa Donee, Attorney au Agent.

Power of Attorney si hati ya “kumkabidhi mtu maisha yako ya kisheria”. Ni chombo cha uwakilishi ambacho mamlaka yake yanatokana na kile kilichoandikwa ndani yake. Kwa hiyo, maneno yaliyomo katika hati hiyo ni muhimu sana.

1. POWER OF ATTORNEY NI NINI?

Power of Attorney ni hati ya kisheria ambayo mtu humpa mwingine mamlaka ya kumwakilisha katika kufanya shughuli maalumu au mbalimbali kwa niaba yake.

Mfano:

ยซAmina anaishi Tanzania lakini ana nyumba Dar es Salaam ambayo anataka kuiuza. Kwa sababu yuko nje ya nchi, anamteua Juma kwa Power of Attorney kumwakilisha katika taratibu za mauzo, kusaini nyaraka na kukamilisha usajili wa muamala.ยป

Katika mfano huo:

– Amina ni Donor/Principal;
– Juma ni Donee/Attorney/Agent;
– Hati inayompa Juma mamlaka ni Power of Attorney.

Kwa hiyo, Power of Attorney hujenga uhusiano wa uwakilishi kati ya Principal na Agent.

2. POWER OF ATTORNEY SI UHAMISHO WA UMILIKI

Hili ni jambo muhimu sana kueleweka.

Kumpa mtu Power of Attorney hakumaanishi kwamba umemhamishia mali yako.

Kwa mfano, kama mwenye nyumba anampa mtu Power of Attorney ya kuuza nyumba, mamlaka hayo hayamaanishi kwamba nyumba imekuwa mali ya huyo Agent.

Agent anakuwa na mamlaka ya kumwakilisha mwenye mali kwa mujibu wa masharti ya Power of Attorney.

Hivyo:

Power of Attorney is not Transfer of Ownership.

Ikiwa Agent ametumia Power of Attorney kuuza ardhi, bado kutakuwa na taratibu za kisheria za transfer na registration ya disposition husika.

Chini ya Land Registration Act, disposition ya registered land inapaswa kusajiliwa na Registrar ili iwe na athari ya kisheria inayotakiwa katika kuunda, kuhamisha, kubadilisha au kufuta interest katika registered land.

3. NANI ANAWEZA KUTOA POWER OF ATTORNEY?

Kwa ujumla, mtu anayetoa Power of Attorney lazima awe na uwezo wa kisheria wa kufanya shughuli anazokusudia kumpa Agent.

Kwa mfano, mtu anayekusudia kumpa mwingine mamlaka ya kuuza ardhi yake lazima awe na mamlaka halali juu ya ardhi hiyo na awe na uwezo wa kisheria wa kuingia katika muamala huo.

Katika kuandaa Power of Attorney, ni muhimu kuangalia:

1. Utambulisho wa Principal;
2. Uwezo wake wa kisheria;
3. Utambulisho wa Agent;
4. Shughuli anazoruhusiwa kufanya Agent;
5. Mali au jambo linalohusika;
6. Muda wa mamlaka;
7. Masharti yoyote maalumu yaliyowekwa na Principal.

4. NANI ANAWEZA KUPEWA POWER OF ATTORNEY?

Kwa kawaida, mtu anaweza kumteua mtu mwingine anayemwamini kuwa Agent wake.

Agent anaweza kuwa, kwa mfano:

– ndugu;
– rafiki;
– mshirika wa biashara;
– mfanyakazi;
– mwanasheria;
– mtu mwingine mwenye uwezo wa kutekeleza shughuli husika.

Hata hivyo, uteuzi wa Agent unapaswa kufanywa kwa tahadhari.

Sababu ni rahisi: Agent anaweza kuwa na uwezo wa kuingia katika miamala yenye madhara makubwa kwa Principal ikiwa Power of Attorney imeandikwa kwa upana sana.

Kwa hiyo, si busara kumpa mtu mamlaka makubwa bila kuweka mipaka yake.

5. POWER OF ATTORNEY INATUMIKA KWA SHUGHULI ZIPI?

Power of Attorney inaweza kutumika katika mazingira mbalimbali kulingana na mamlaka yaliyotolewa.

Baadhi ya matumizi yake ni:

(a) Kushughulikia mali

Mtu anaweza kumteua Agent:

– kusimamia nyumba;
– kukusanya kodi;
– kusaini mikataba;
– kushughulikia hati;
– kufuatilia taratibu za ardhi;
– kufanya maombi mbalimbali kuhusu mali.

(b) Mauzo ya mali

Principal anaweza kumpa Agent mamlaka ya:

– kutafuta mnunuzi;
– kujadiliana masharti;
– kusaini mkataba wa mauzo;
– kuwasilisha nyaraka;
– kufuatilia transfer;
– kukamilisha taratibu za usajili.

Hata hivyo, Power of Attorney inapaswa kueleza kwa uwazi mamlaka hayo.

(c) Masuala ya ardhi

Power of Attorney inaweza kutumika katika:

– transfer;
– mortgage;
– discharge;
– registration;
– applications;
– kushughulikia nyaraka za ardhi;
– shughuli nyingine zinazoruhusiwa na mamlaka yaliyotolewa.

Kwa registered land, Land Registration Act ina masharti maalumu kuhusu matumizi na filing ya Power of Attorney.

(d) Biashara

Mmiliki wa biashara anaweza kumteua mtu:

– kusaini nyaraka;
– kufanya mawasiliano;
– kushughulikia miamala;
– kuwakilisha biashara katika shughuli fulani.

Lakini mamlaka ya Agent yatategemea namna Power of Attorney ilivyoandikwa na aina ya taasisi au muamala unaohusika.

(e) Mashauri ya kiraia

Power of Attorney inaweza pia kuwa muhimu katika uwakilishi katika masuala ya kiraia, kwa mujibu wa sheria na taratibu husika za mahakama.

Hata hivyo, ni muhimu kutofautisha kati ya Power of Attorney ya jumla ya uwakilishi na masharti maalumu yanayohusu nani anaweza kuonekana au kufanya jambo fulani mahakamani.

6. AINA ZA POWER OF ATTORNEY

Hakuna maana kwamba kila Power of Attorney inapaswa kuwa na mamlaka sawa.

Kwa matumizi ya kawaida, tunaweza kueleza aina zake kwa kuangalia upana wa mamlaka.

(A) General Power of Attorney

Hii humpa Agent mamlaka mapana ya kushughulikia mambo mbalimbali kwa niaba ya Principal.

Kwa mfano, inaweza kumpa Agent mamlaka ya:

– kusimamia mali;
– kusaini nyaraka;
– kushughulikia biashara;
– kufanya maombi;
– kuwasiliana na taasisi;
– kufanya miamala mbalimbali.

Kwa sababu ya upana wake, General Power of Attorney inahitaji tahadhari kubwa wakati wa kuandaliwa.

(B) Special Power of Attorney

Hii humpa Agent mamlaka ya kufanya jambo maalumu au shughuli maalumu.

Mfano:

ยซ”Ninampa Juma mamlaka ya kuniwakilisha katika kuuza kiwanja changu kilichopo…”ยป

Hii ni salama zaidi pale Principal anapotaka mamlaka ya Agent yaishie kwenye shughuli fulani.

Kwa mfano, badala ya kusema:

ยซ”Agent ana mamlaka ya kushughulikia mali zangu zote.”ยป

Unaweza kueleza:

ยซ”Agent ana mamlaka ya kushughulikia uuzaji wa kiwanja kinachotambulika kwa…”ยป

Tofauti hiyo inaweza kuwa muhimu sana kisheria.

7. POWER OF ATTORNEY YA ARDHI

Hili ni eneo linalohitaji umakini zaidi.

Kwa mujibu wa section 95 ya Land Registration Act, Cap. 334, pale ambapo mtu anasaini application au deed kama Agent wa mtu mwingine katika shughuli zinazohitaji usajili chini ya sheria hiyo, hati hiyo haiwezi kukubaliwa kwa registration isipokuwa Agent awe ameidhinishwa kwa Power of Attorney iliyotekelezwa na kushuhudiwa kwa namna inayotakiwa kwa deeds.

Hii ina maana kwamba si kila Power of Attorney ya kawaida inaweza kutumika moja kwa moja katika kila transaction ya registered land.

8. USAJILI WA POWER OF ATTORNEY INAYOHUSU REGISTERED LAND

Section 96 ya Land Registration Act ni muhimu sana.

Ikiwa Power of Attorney ina mamlaka ya kufanya applications chini ya Act kwa ajili ya:

– disposition ya registered land; au
– kutenda mambo mengine yanayohusiana na registered land,

Registrar anatakiwa ku-file Power of Attorney hiyo baada ya joint application ya donor na donee, kwa kufuata masharti ya sheria.

Kwa hiyo, katika shughuli za registered land, suala la Power of Attorney halipaswi kuangaliwa kama jambo la kawaida tu la “kusaini karatasi”.

Lazima izingatiwe kama sehemu ya mfumo wa usajili wa ardhi.

9. POWER OF ATTORNEY INASAINIWAJE?

Power of Attorney inapaswa kuandaliwa kwa namna inayokidhi mahitaji ya kisheria na aina ya transaction inayokusudiwa.

Kwa Power of Attorney inayohusiana na registered land, sheria inaelekeza kwamba utekelezaji na attestation yake ufuate masharti yanayotumika kwa deeds chini ya sections 92 na 93 za Land Registration Act.

Kwa hiyo, si busara kutumia template ya mtandaoni bila kuangalia:

– aina ya transaction;
– aina ya mali;
– mamlaka yanayotolewa;
– mahali Power of Attorney inatekelezwa;
– mahitaji ya usajili;
– taasisi itakayotumia hati hiyo.

10. USAJILI WA POWER OF ATTORNEY TANZANIA

Kwa upande wa usajili wa nyaraka, Wizara yenye dhamana ya Ardhi inaeleza kwamba chini ya Registration of Documents Act, Cap. 117, Power of Attorney iko miongoni mwa nyaraka zinazoweza kufanyiwa optional registration.

Hii inapaswa kutofautishwa na hali ya registered land chini ya Land Registration Act.

Kwa hiyo, kuna tofauti kati ya:

Optional registration

Power of Attorney inaweza kusajiliwa kwa mfumo wa Registration of Documents Act katika mazingira yanayohusika.

Mandatory filing katika registered land

Ikiwa Power of Attorney ina mamlaka yanayohusiana na disposition au shughuli nyingine kuhusu registered land, section 96 ya Land Registration Act inaweka utaratibu maalumu wa filing yake kwa Registrar.

Kwa hiyo, kusema tu kwamba:

ยซ”Power of Attorney Tanzania si lazima kusajiliwa”ยป

ni kauli pana sana na inaweza kumpotosha mtu.

Lazima kwanza ujue Power of Attorney hiyo inatumika kwa jambo gani.

11. USAJILI CHINI YA REGISTRATION OF DOCUMENTS ACT

Registration of Documents Act, Cap. 117, ni sheria inayohusu registration ya nyaraka mbalimbali.

Sheria hiyo inaweka mfumo wa compulsory registration kwa nyaraka fulani na pia ina utaratibu wa kuwasilisha nyaraka kwa usajili.

Wizara ya Ardhi pia inaeleza Power of Attorney kama moja ya nyaraka zinazoweza kusajiliwa kwa hiari chini ya mfumo wa Registration of Documents Act.

Kwa hiyo, mtu anayehitaji kusajili Power of Attorney anapaswa kwanza kutambua ni mfumo gani wa usajili unaotumika kulingana na matumizi ya hati hiyo.

12. POWER OF ATTORNEY INAHITAJIWA KUWA REGISTERED?

Jibu ni:

Inategemea matumizi yake.

Ikiwa Power of Attorney ni ya shughuli ya kawaida, usajili wake unaweza kutegemea aina ya nyaraka na mahitaji ya taasisi au transaction husika.

Lakini ikiwa inahusu registered land na ina mamlaka ya kufanya disposition au kushughulikia mambo chini ya Land Registration Act, section 96 inakuwa muhimu na Power of Attorney hiyo inapaswa kufanyiwa filing kwa Registrar kwa mujibu wa sheria.

Hivyo, kabla ya kutumia Power of Attorney katika transaction kubwa, ni muhimu kuthibitisha mahitaji ya usajili ya transaction hiyo.

13. POWER OF ATTORNEY INAWEZA KUFUTWA?

Ndiyo.

Principal anaweza kuondoa au revoke mamlaka aliyompa Agent, isipokuwa pale ambapo sheria au masharti ya Power of Attorney yenyewe yanaweka hali maalumu, kama Power of Attorney iliyotolewa kwa consideration na kuonyeshwa kuwa irrevocable.

Kwa registered land, section 96 inaweka utaratibu wa kutoa notice ya revocation kwa Registrar. Registrar anaweza ku-file notice hiyo na kuonyesha revocation kwenye Power of Attorney iliyofanyiwa filing.

Pia sheria inatambua mazingira kama:

– kifo;
– bankruptcy;
– disability

ya donor au, katika mazingira yanayotajwa na sheria, donee, kama sababu zinazoweza kuathiri kuendelea kwa Power of Attorney.

14. JE, POWER OF ATTORNEY HUISHIA KIFO CHA DONOR?

Kwa kawaida, Power of Attorney haiwezi kuchukuliwa kama chombo cha kuendeleza mamlaka baada ya kifo cha Principal bila kuangalia sheria na mazingira maalumu ya mamlaka hiyo.

Kifo cha Principal ni tukio kubwa la kisheria linaloweza kumaliza authority ya Agent.

Baada ya kifo, masuala ya mali ya marehemu yanaingia katika mfumo wa probate na administration of estates.

Hivyo, Power of Attorney si mbadala wa:

– Will;
– Probate;
– Letters of Administration;
– succession proceedings.

Kwa mfano, mtu hawezi kusema:

ยซ”Marehemu alinipa Power of Attorney, kwa hiyo mimi ndiye nitasimamia mali zake milele.”ยป

Hilo si jambo la kuchukuliwa kirahisi.

15. POWER OF ATTORNEY NA WOSIA NI TOFAUTI

Hati hizi mbili mara nyingi huchanganywa, lakini zina kazi tofauti.

Power of Attorney

Hutumika kumpa mtu mamlaka ya kukuwakilisha ukiwa hai, kwa mujibu wa masharti yake.

Will

Ni tamko la mtu kuhusu namna mali yake itakavyoshughulikiwa baada ya kifo, kwa mujibu wa sheria husika.

Kwa hiyo:

Power of Attorney si Will.

Na:

Agent si lazima awe beneficiary wa mali ya Principal.

16. POWER OF ATTORNEY NA SALE AGREEMENT NI TOFAUTI

Power of Attorney pia si mkataba wa mauziano.

Mfano:

Mmiliki wa ardhi anamteua Juma kwa Power of Attorney kuuza ardhi.

Power of Attorney inampa Juma authority to act.

Lakini mkataba wa mauziano ndio unaweka masharti ya transaction ya mauziano, na transfer/disposition inayohusika inapaswa kukidhi masharti ya sheria.

Kwa registered land, disposition inahitaji registration kwa Registrar.

17. HATARI ZA POWER OF ATTORNEY ILIYOANDIKWA VIBAYA

Power of Attorney inaweza kuwa chombo muhimu sana, lakini inaweza pia kuwa chanzo cha migogoro ikiwa imeandikwa bila mipaka.

Baadhi ya hatari ni:

1. Mamlaka kuwa mapana kupita kiasi

Principal anaweza kumpa Agent uwezo wa kufanya miamala mingi kuliko alivyokusudia.

2. Kutokutaja mali husika

Badala ya kutaja property maalumu, hati ikaandika “all my properties”.

Hii inaweza kuleta matatizo makubwa.

3. Kutokuweka muda

Power of Attorney isiyo na mipaka ya muda inaweza kuleta maswali kuhusu iwapo bado inaendelea.

4. Agent kutumia mamlaka kinyume na instructions

Agent anaweza kufanya transaction ambayo Principal hakukusudia.

5. Kutokutoa notice ya revocation

Principal akifuta Power of Attorney lakini hakufuata utaratibu unaohitajika wa kuwajulisha wahusika au Registrar katika mazingira husika, matatizo yanaweza kutokea.

Kwa registered land, sheria inaweka utaratibu maalumu wa notice ya revocation na athari zake.

18. PRINCIPAL ANAPASWA KUWEKA MIPAKA GANI?

Power of Attorney nzuri inapaswa kuonyesha kwa uwazi:

Nani?

Principal na Agent ni akina nani?

Kwa jambo gani?

Ni shughuli gani Agent anaruhusiwa kufanya?

Kwa mali gani?

Mali husika itambulike kwa usahihi.

Kwa muda gani?

Mamlaka yaanze lini na, inapofaa, yaishe lini?

Kwa masharti gani?

Kuna masharti maalumu ambayo Agent lazima ayafuate?

Je, Agent anaweza kumteua mtu mwingine?

Hili lisiachwe bila kufikiriwa ikiwa ni muhimu kwa transaction.

19. POWER OF ATTORNEY YA KUUZA ARDHI

Hili ni eneo ambalo tahadhari inahitajika zaidi.

Ikiwa Principal anataka Agent kuuza ardhi, Power of Attorney inapaswa kueleza kwa uwazi:

1. maelezo ya Principal;
2. maelezo ya Agent;
3. maelezo ya ardhi;
4. mamlaka ya kutangaza au kutafuta mnunuzi;
5. mamlaka ya kujadiliana;
6. mamlaka ya kusaini mkataba pale inapohitajika;
7. mamlaka ya kushughulikia transfer;
8. mamlaka ya kuwasilisha nyaraka;
9. masharti yoyote kuhusu bei;
10. muda wa mamlaka.

Ikiwa ni registered land, mahitaji ya Land Registration Act kuhusu Agent na filing ya Power of Attorney yanapaswa kuzingatiwa.

20. JE, AGENT ANAWEZA KUUZA MALI YA PRINCIPAL KWAKE MWENYEWE?

Hili ni eneo nyeti sana.

Ikiwa Agent amepewa mamlaka ya kuuza mali na akajiuza mwenyewe, kuna uwezekano mkubwa wa kuzuka maswali kuhusu conflict of interest, fiduciary obligations, authority na uhalali wa transaction.

Kwa hiyo, kama Principal anakusudia kuruhusu transaction ya aina hiyo, jambo hilo linapaswa kuandikwa kwa uwazi sana na kufanyiwa tathmini ya kisheria kabla ya transaction.

Kanuni salama ni:

ยซAgent hatakiwi kutumia mamlaka aliyopewa kwa namna inayokiuka maslahi au instructions za Principal.ยป

21. POWER OF ATTORNEY INAYOTOLEWA NJE YA TANZANIA

Mtanzania au mtu mwingine aliye nje ya Tanzania anaweza kuhitaji kumpa mtu aliye Tanzania mamlaka ya kumwakilisha.

Katika mazingira hayo, suala la:

– execution;
– witnessing;
– authentication;
– notarisation;
– legalisation;
– matumizi ya hati nchini Tanzania

linapaswa kuangaliwa kwa makini.

Hasa ikiwa Power of Attorney itatumika katika transaction ya ardhi, si busara kudhani kwamba hati iliyosainiwa nje ya Tanzania itakubalika moja kwa moja bila kufuata formalities zinazohitajika.

22. POWER OF ATTORNEY NA MWANASHERIA

Kumteua mwanasheria kama Agent kunaweza kuwa na manufaa katika shughuli zinazohitaji uelewa wa kisheria.

Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kwamba:

Power of Attorney haibadilishi sheria za professional representation.

Kwa mfano, katika shughuli za mahakama, sheria za procedural representation na legal practice bado zinatumika.

Kwa hiyo, kumpa mtu Power of Attorney hakumaanishi moja kwa moja kwamba anaweza kufanya kila jambo mahakamani ambalo kwa sheria linapaswa kufanywa na Advocate au mtu mwingine mwenye sifa zinazotakiwa.

23. HATUA ZA KUANDAA POWER OF ATTORNEY

Kwa ujumla, mchakato mzuri unaweza kufuata hatua hizi:

Hatua ya 1: Tambua lengo

Eleza kwa nini Power of Attorney inahitajika.

Hatua ya 2: Tambua Principal

Thibitisha utambulisho wa mtu anayetoa mamlaka.

Hatua ya 3: Chagua Agent

Chagua mtu anayeaminika na mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu.

Hatua ya 4: Bainisha mamlaka

Usitumie maneno mapana yasiyo na sababu.

Hatua ya 5: Tambua mali au transaction

Ikiwa ni ardhi, eleza particulars zake kwa usahihi.

Hatua ya 6: Andaa hati

Hati iandaliwe kwa kuzingatia aina ya transaction na sheria husika.

Hatua ya 7: Execute na attest

Saini na ushuhudiwe kwa namna inayotakiwa kisheria.

Hatua ya 8: Sajili/file inapohitajika

Ikiwa transaction iko chini ya Land Registration Act, zingatia section 96 na taratibu za Registrar.

Hatua ya 9: Agent atekeleze mamlaka

Agent afanye tu yale yaliyo ndani ya scope ya Power of Attorney.

24. NYARAKA MUHIMU ZA KUZINGATIA

Mahitaji yanaweza kutofautiana kulingana na transaction, lakini kwa kawaida ni muhimu kuwa na:

– kitambulisho halali cha Principal;
– kitambulisho cha Agent;
– Power of Attorney iliyotekelezwa;
– nyaraka za mali husika;
– Certificate of Title au nyaraka nyingine za ardhi inapohusika;
– nyaraka za transaction;
– ushahidi mwingine unaohitajika na Registrar au taasisi husika.

Ni muhimu kuthibitisha mahitaji ya sasa ya ofisi inayohusika kabla ya kuwasilisha nyaraka.

25. POWER OF ATTORNEY NA REGISTRAR OF TITLES

Katika masuala ya registered land, Registrar ana jukumu muhimu.

Land Registration Act inaweka kwamba Registrar anaweza kufile Power of Attorney inayokidhi masharti ya section 96.

Pia, endapo revocation imewasilishwa kwa mujibu wa sheria, Registrar anaweza kuifile na kuonyesha revocation hiyo kwenye Power of Attorney.

Hii inalenga kuweka rekodi rasmi kuhusu mamlaka ya Agent.

26. JE, POWER OF ATTORNEY INAWEZA KUTUMIKA BAADA YA KUFUTWA?

Kwa kawaida, Agent hapaswi kuendelea kutumia mamlaka ambayo tayari yamefutwa.

Katika registered land, section 96 inaweka utaratibu ambao Registrar anaweza kukataa document iliyosainiwa na Agent ikiwa notice ya revocation imewasilishwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa hiyo, mtu anayefanya transaction na Agent anapaswa kuwa makini pia kuhusu suala la authority.

27. PRINCIPAL ANAPASWA KUWA MAKINI NA NINI?

Kabla ya kusaini Power of Attorney:

Usimpe mtu mamlaka usiyoyahitaji.

Usitumie General Power of Attorney kama Special Power of Attorney inatosha.

Eleza property kwa usahihi.

Weka mipaka ya mamlaka.

Weka muda inapofaa.

Eleza kama Agent anaweza au hawezi delegate authority.

Eleza masharti ya fedha pale inapohusika.

Hifadhi original salama.

Ikiwa ni ardhi, hakikisha taratibu za Land Registration Act zimefuatwa.

28. AGENT ANAPASWA KUWA MAKINI NA NINI?

Agent naye ana wajibu wa kutumia mamlaka kwa uaminifu na ndani ya scope aliyopewa.

Agent hapaswi kudhani:

ยซ”Nimepewa Power of Attorney, kwa hiyo naweza kufanya chochote.”ยป

Hilo ni kosa.

Authority ya Agent inatokana na Power of Attorney.

Ikiwa hati inasema:

ยซ”Sell Plot A”ยป

si busara Agent kuuza Plot B kwa sababu tu anasimamia mali zote za Principal.

Mamlaka yanapaswa kusomwa kwa uangalifu.

29. HITIMISHO
Power of Attorney ni chombo muhimu cha kisheria kinachomwezesha mtu kumteua mwingine kumwakilisha katika shughuli mbalimbali. Hata hivyo, Power of Attorney si hati ya kumpa Agent umiliki wa mali. Ni hati ya kumpa mamlaka ya uwakilishi.

Katika Tanzania, suala la usajili linahitaji kuangaliwa kwa kutofautisha kati ya mfumo wa Registration of Documents Act, Cap. 117 na masharti maalumu ya Land Registration Act, Cap. 334, hasa pale Power of Attorney inapohusu registered land. Wizara ya Ardhi yenyewe inaeleza Power of Attorney kama nyaraka inayoweza kufanyiwa optional registration chini ya Registration of Documents Act, wakati section 96 ya Land Registration Act inaweka utaratibu maalumu wa filing kwa Power of Attorney inayohusu registered land.


Discover more from ๐‹๐„๐†๐€๐‹๐‰๐€๐Œ๐ˆ๐ˆโš–๏ธ

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Published by LEGALJAMIIโš–๏ธ

Richard Kalokola is a Tanzanian legal professional with a Bachelor of Laws (LL.B) from St. Augustine University of Tanzania and professional training from the Law School of Tanzania. He has a strong passion for legal education, research, and public legal awareness. As the founder of LegalJamii, Richard is dedicated to bridging the gap between complex legal principles and everyday understanding by delivering accurate, practical, and accessible legal information. His vision is to promote a legally informed society where individuals, businesses, and communities can confidently understand their rights, responsibilities, and available legal solutions. Through LegalJamii, he continues to advance legal literacy by transforming legal concepts into clear and simplified language for the benefit of the wider public.

Leave a Reply

Discover more from ๐‹๐„๐†๐€๐‹๐‰๐€๐Œ๐ˆ๐ˆโš–๏ธ

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Discover more from ๐‹๐„๐†๐€๐‹๐‰๐€๐Œ๐ˆ๐ˆโš–๏ธ

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading