HURIDHIKI NA MAKADIRIO YA KODI? SHERIA ZA KODI TANZANIA ZINASEMAJE NA UFANYE NINI?


Na LegalJamii

Kodi si mzigo.


Kodi ni chanzo kikuu cha mapato ya serikali na msingi wa utoaji wa huduma za jamii. Lakini kwa upande wa mlipakodi, kodi ni pia eneo linalohitaji uwazi, haki, na usawa wa kisheria. Ndiyo maana mfumo wa kodi Tanzania umeweka taratibu maalum za kuhakikisha mlipakodi halipishwi kodi isiyo sahihi au isiyo halali.


Makala hii inaeleza kwa ufupi mfumo wa sheria za kodi Tanzania na hatua za kuchukua pale mlipakodi asiporidhika na makadirio ya kodi, kwa mujibu wa sheria.


1. Mfumo wa Sheria za Kodi Tanzania

Sheria kuu zinazosimamia   masuala ya kodi ni:

Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438 (Tax Administration Act, TAA)

Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura ya 332 (Income Tax Act)

Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, Sura ya 148 (VAT Act)

Sheria ya Ushuru wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa (EAC Customs Management Act na Excise Duty Act)


Kwa mujibu wa Kifungu cha 15 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndiyo yenye jukumu la kusimamia, kukusanya, na kutekeleza sheria zote za kodi nchini.


2. Maana ya Makadirio ya Kodi Kisheria.


Makadirio ya kodi ni uamuzi wa TRA unaobainisha kiasi cha kodi kinachodaiwa na mlipakodi. Kwa mujibu wa Kifungu cha 3(3) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Kamishna anaweza kutoa makadirio pale ambapo:


Mlipakodi ameshindwa kuwasilisha taarifa za kodi kwa wakati, au


Taarifa zilizowasilishwa si sahihi au hazijitoshelezi.


Sheria inaruhusu hata makadirio ya kubahatisha (best judgment assessment), lakini lazima yazingatie taarifa zilizopo na misingi ya haki ya kiutawala.


3. Haki za Mlipakodi Chini ya Sheria.


Sheria za kodi Tanzania zimempa mlipakodi haki muhimu, ikiwemo:


Haki ya kupewa taarifa na sababu za makadirio (Kifungu cha 49, TAA),


Haki ya kusikilizwa kabla ya uamuzi wa mwisho.


Haki ya kupinga makadirio yasiyo sahihi (Kifungu cha 51, TAA),


Haki ya kukata rufaa kwa vyombo vya haki (Sheria ya Bodi za Rufaa za Kodi, Sura ya 408).


Haki ya kukata rufaa kwa vyombo vya haki (Sheria ya Bodi za Rufaa za Kodi, Sura ya 408).


Kwa lugha nyepesi: kodi ni wajibu wa kisheria, lakini kulipishwa kodi isiyo sahihi si sehemu ya mfumo halali wa sheria.


4. Nini Cha Kufanya Kama Huridhiki na Makadirio ya Kodi.


(a) Kuwasilisha Pingamizi kwa Kamishna Mkuu wa TRA
Kwa mujibu wa Kifungu cha 51(1) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi, mlipakodi anaweza kuwasilisha pingamizi kwa maandishi ndani ya siku 30 tangu kupokea notisi ya makadirio.
Pingamizi hilo lazima:
Lieleze wazi sababu za kutoridhika (Kifungu cha 51(2)),
Liambatanishwe na vielelezo,
Lizingatie sharti la kulipa kodi isiyopingwa au moja ya tatu(1/3) ya makadirio yote, kiasi chochote kitakachokuwa kikubwa. (Kifungu cha 51(5)).
Kwa kifupi: huwezi kupinga kodi kwa hisia โ€” lazima kwa hoja na ushahidi.


(b) Rufaa kwa Bodi ya Rufaa ya Kodi (Tax Revenue Appeals Board โ€“ TRAB)
Endapo mlipakodi hajaridhika na uamuzi wa Kamishna kuhusu pingamizi, anaweza kukata rufaa TRAB ndani ya siku 30 kwa mujibu wa Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Bodi za Rufaa za Kodi, Sura ya 408.


(c) Rufaa kwa Baraza la Rufaa ya Kodi (Tax Revenue Appeals Tribunal โ€“ TRAT)
Kwa mujibu wa Kifungu cha 16(4) cha Sheria ya Bodi za Rufaa za Kodi, mlipakodi anaweza kukata rufaa TRAT endapo hajaridhika na uamuzi wa TRAB.


(d) Rufaa kwa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania
Hatua ya mwisho ni kukata rufaa Mahakama ya Rufaa kwa masuala ya kisheria pekee (points of law), kwa mujibu wa Kifungu cha 25 cha Sheria ya Bodi za Rufaa za Kodi.


Kwa maneno mengine: safari ya kodi inaweza kuanzia TRA na kuishia Mahakama ya Rufaa lakini mara nyingi haki hupatikana kabla ya hapo kama hoja zimeandaliwa vizuri.


5. Umuhimu wa Kuzingatia Muda na Taratibu
Sheria za kodi ni kali kuhusu muda. Pingamizi au rufaa ikichelewa, hata kama hoja zako ni nzito kama risala ya uzamivu, zinaweza kukosa kusikilizwa kwa sababu ya taratibu pekee.
Ndiyo maana Kifungu cha 52(1) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi kinampa Kamishna mamlaka ya kukataa pingamizi lisilokidhi masharti ya kisheria.
Kwa kifupi: haki inampendelea aliye makini si aliye na hoja nzuri pekee.


6. Changamoto za Kivitendo kwa Walipakodi
Katika vitendo, walipakodi hukumbana na:
Uelewa mdogo wa sheria za kodi, Hofu ya migogoro na mamlaka za kodi, Gharama za uwakilishi wa kisheria, Ucheleweshaji wa maamuzi.


Lakini ikumbukwe: mfumo wa kodi haukusudiwi kuwa adhabu bali ni ushirikiano wa kimaendeleo. Migogoro ikisimamiwa kitaalamu, hutatuliwa bila โ€œkupandisha presha ya moyo wala ya akaunti ya benki.โ€


7. Hitimisho.


Sheria za kodi Tanzania zimejengwa juu ya misingi ya haki, uwazi, na uwajibikaji. Mlipakodi ana wajibu wa kulipa kodi stahiki, lakini pia ana haki ya kupinga makadirio yasiyo sahihi kwa kutumia njia za kisheria zilizowekwa.


Kwa lugha ya LegalJamii:
Kodi ni wajibu wa kisheria lakini dhuluma si sehemu ya mfumo. Na kama makadirio yamekuzidia, usikate tamaa, Weka pingamizi kwa maandishi, kwa muda, na kwa hoja.


Discover more from ๐‹๐„๐†๐€๐‹๐‰๐€๐Œ๐ˆ๐ˆโš–๏ธ

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Published by LEGALJAMIIโš–๏ธ

Richard Kalokola is a Tanzanian legal professional with a Bachelor of Laws (LL.B) from St. Augustine University of Tanzania and professional training from the Law School of Tanzania. He has a strong passion for legal education, research, and public legal awareness. As the founder of LegalJamii, Richard is dedicated to bridging the gap between complex legal principles and everyday understanding by delivering accurate, practical, and accessible legal information. His vision is to promote a legally informed society where individuals, businesses, and communities can confidently understand their rights, responsibilities, and available legal solutions. Through LegalJamii, he continues to advance legal literacy by transforming legal concepts into clear and simplified language for the benefit of the wider public.

Leave a Reply

Discover more from ๐‹๐„๐†๐€๐‹๐‰๐€๐Œ๐ˆ๐ˆโš–๏ธ

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Discover more from ๐‹๐„๐†๐€๐‹๐‰๐€๐Œ๐ˆ๐ˆโš–๏ธ

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading